UNIDO×DMM.Africa Ujuzi wa juu wa Japani kutumika nchi zinazoendelea
「Ziara ya basi ya DMM.make AKIBA」 iliandaliwa

Kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa (UNIDO), DMM.Africa iliandaa ziara ya "DMM.make Akiba" kwa ajili ya wafanyakazi wa ubalozi wa nchi za Afrika, Jumanne Aprili 26, 2016.

「DMM.make Akiba」 inaundwa na 「DMM.make Akiba Base」 ambayo ina ofisi ya kushirikiana na nafasi ya matukio inayoweza kutumika kwa ajili ya kuendeleza biashara, vilevile 「DMM.make Akiba Studio」 ambayo ina vifaa vya kisasa kwa ajili ya kuvumbua na kutengeneza vifaa mbalimbali vya ujenzi.
Hii ni sehemu ambayo ina mazingira yote kwa ajili ya wavumbuzi wa bidhaa mbalimbali.

Siku hiyo, jumla ya wafanyakazi 19 wa ubalozi wa nchi 15, ikiwa ni pamoja na balozi mmoja, walishiriki. Washiriki hawa walionyeshwa vifaa vya kisasa na bidhaa bora zilizotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya printa ya 3D.

Wafanyakazi wa balozi za nchi mbalimbali walisifia kuwepo kwa kituo hichi chenye miundombinu ya kusaidia wajasiriamali wanaotengeneza vifaa mbalimbali vya ujenzi na pia kusema kuwa wanafikiri kuna uwezekano mkubwa wa bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa kwenye kituo hicho kuenea maeneo mbalimbali barani Afrika. 「DMM.make Akiba」 iliweza kujulikana marudufu kupitia ziara hii.

Ziara za UNIDO katika ofisi za 「DMM.make AKIBA」 (*Tovuti ya Kijapani)

DMM.Africa ilianzishwa Septemba 2015 kwa ajili ya kutengeneza biashara ambazo zitakuwa biashara miamba za kundi la DMM. Kutokana na ongezeko kubwa la watu siku zijazo, Soko la barani Afrika litaongezeka mara dufu na DMM.Africa inaanzisha biashara mpya Afrika kwa ajili hii. Mwaka 2016, DMM.Africa pia iliandaa moja ya shindano kubwa la kibiashara linaloitwa DMM.AfricaPresents 【AfricaBusinessIdeaCup】. DMM.Africa inalenga kutafuta na kulea vijana wenye vipaji vya kibiashara, kukuza biashara za wajasiriamali wazuri na kufanya biashara pamoja na wajasiriamali wa Afrika.