Maonesho ya biashara ya Saba Saba

Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam.

Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam hufanyika mwezi wa saba kila mwaka. Ikiwa ni moja kati ya maonesho makubwa zaidi ya kibiashara barani Afrika, ikifanya maadhimisho ya miaka 40 mwaka 2016.
Tarehe 7 Julai, siku ambayo maonesho haya yanajivunia wahudhuriaji wengi sana, ni siku ya mapumziko kitaifa.
Kwa kiswahili, lugha mama ya Tanzania, namba 7 inatamkwa kama “Saba”, na hivyo maonesho haya yanajulikana na watu wengi kwa jina maarufu la “SabaSaba”. Takribani makampuni 1000 kutoka ndani na nje ya Tanzania hufanya maonesho ya sekta mbali mbali ikiwemo Chakula, Vifaa vya Umeme, Mashine za Kilimo, Vifaa vya Ofisini na vingine vingi.
Takribani watu 200,000 huudhuria maonesho haya ya biashara jijini Dar es Salaam, na hivyo kuifanya hii kuwa ni nafasi nzuri sana kwa wanaoshiriki kuonesha bidhaa zao kutambulika nchini tanzania kwa bidhaa na huduma zao.

Shughuli za DMM.Africa

Bidhaa bora kabisa zilizotengenezwa na kitengo chetu cha zilionyeshwa kwenye maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba.
Hii ilikuwa ni nafasi murua kabisa kuona kama bidhaa hizi bora kutoka Japani zitapendwa na watu wa Afrika, pamoja na kutafuta washiliki wa kuweza kuzitawanya na kuziuza bidhaa hizi.

Mwongozo wa maonesho ya kimataifa ya biashara
Dar es Salaam mwaka 2016.

Tarehe: 2016/7/1~2016/7/7 (siku 7)
Mahali: Dar es Salaam, United Republic of Tanzania
Ukumbi: Viwanja vya maonesho ya biashara vya Mwalimu J.K Nyerere
Mwenyeji: Tanzania Trade Development Authority (TANTRADE)
Eneo la maonesho: Mita za mraba 35,000 (Eneo zima: Mita za mraba 160,000)
Idadi ya washiriki: Takribani makampuni, vyuo na mashirika 1,000
Sekta zilizolengwa: Maonesho ya kina ya kibiashara
(Chakula, bidhaa nyinginezo, vifaa vya elektroniki, magari, huduma za kifedha nakadhalika)
Idadi ya wageni: Takribani watu 220,000( Namba iliyotolea kwenye orodha rasmi mwaka 2014)

DMM.Africa ilianzishwa Septemba 2015 kwa ajili ya kutengeneza biashara ambazo zitakuwa biashara miamba za kundi la DMM. Kutokana na ongezeko kubwa la watu siku zijazo, Soko la barani Afrika litaongezeka mara dufu na DMM.Africa inaanzisha biashara mpya Afrika kwa ajili hii. Mwaka 2016, DMM.Africa pia iliandaa moja ya shindano kubwa la kibiashara linaloitwa DMM.AfricaPresents 【AfricaBusinessIdeaCup】. DMM.Africa inalenga kutafuta na kulea vijana wenye vipaji vya kibiashara, kukuza biashara za wajasiriamali wazuri na kufanya biashara pamoja na wajasiriamali wa Afrika.