ABIC:Africa Business Idea Cup

Kikombe cha Wazo la
Kibiashara kutoka Afrika

Mashindano za mawazo za kibiashara ilifanywa kutoka mwezi wa Nne hadi mwezi wa Saba 2016, katika nchi za: Kenya, Rwanda, Zambia, Zimbabwe na Tanzania.

Filamu kuhusu Shindano la Wazo la Kibiashara Afrika ( English 2:34 )

Zawadi kubwa

Tiketi za ndege kwenda Japani
+
$ 5,000

Mwakilishi wa Kenya, Angela W. Wanjohi ndiye aliyepatikana mshindi.
Mshindi huyu alitambulishwa kwa waandishi wa habari Tokyo wakati alipotembelea Japani

DHANA

Rwanda, Kenya, Tanzania, Zambia, Zimbabwe

Kwa kuzingatia hali iliyopo ya wasomi wengi kuondoka Afrika, DMM.com itawasaidia vijana wanaotaka kujipanga na kuwekeza katika nchi zao, sio tu kwa uwekezaji wa kifedha bali pia na msaada wa karibu wa kibiashara.
Kikombe cha wazo la kibiashara kutoka Afrika ni shindano kubwa linalojumuisha nchi tano ambapo mshindi atazawadiwa tiketi za kwenda Japani na dola za kimarekani elfu tano ($5000) na ubia/ushirikiano wa kibiashara na kampuni bunifu ya kijapani, DMM.com

HATUA ZA SHINDANO LA KIBIASHARA

 • Mwanzo

 • Hatua ya kwanza (Mchujo wa waombaji)
  Vigezo vya msingi: “Uasilia, Uhitaji na Umakini”
 • Kipindi na washauri wetu
  Mshauri mmoja atafanya kazi na kila timu ili kuboresha mipango yao ya awali ya biashara.
 • Hatua ya pili (kuwasilisha)
  Pamoja na vigezo vya mchujo vya “utengenezaji faida, urahisi wa kufanyika na malengo ya baadaye” pia utu na uwezo wa muhusika utazingatiwa.
 • Mwisho
  Mawasilisho ya mwisho ya pamoja.
 • Kutangaza Matokeo.

Download PDF ( English )

DMM.Africa ilianzishwa Septemba 2015 kwa ajili ya kutengeneza biashara ambazo zitakuwa biashara miamba za kundi la DMM. Kutokana na ongezeko kubwa la watu siku zijazo, Soko la barani Afrika litaongezeka mara dufu na DMM.Africa inaanzisha biashara mpya Afrika kwa ajili hii. Mwaka 2016, DMM.Africa pia iliandaa moja ya shindano kubwa la kibiashara linaloitwa DMM.AfricaPresents 【AfricaBusinessIdeaCup】. DMM.Africa inalenga kutafuta na kulea vijana wenye vipaji vya kibiashara, kukuza biashara za wajasiriamali wazuri na kufanya biashara pamoja na wajasiriamali wa Afrika.